1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia kutoshiriki duru ya mwisho ya mazungumzo ya Nile

26 Februari 2020

Ethiopia haitashiriki duru ya mwisho ya mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani na yanayotarajiwa kufanyika wiki hii kuhusu mzozo juu ya mradi wa bwawa la umeme  katika mto Nile kati yake na Misri na Sudan.

https://p.dw.com/p/3YSuv
BG Grand Renaissance Dam | Der äthiopische Premierminister Abiy Ahmed Ali mit dem ägyptischen Präsident Abdel-Fattah al-Sisi (2018)
Picha: Imago Images/Xinhua

Wizara ya maji ya Ethiopia imesema hayo siku ya Jumatano. Makubaliano ya mwisho kuhusu mradi wa bwawa kubwa kabisa la umeme yalitarajiwa kufikiwa mwezi huu, lakini waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema kwenye ziara yake wiki iliyopita nchini Ethiopia kwamba makubaliano hayo sasa yanaweza kuchukua miezi kadhaa kwa kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanywa. Ethiopia haitashiriki mazungumzo hayo yanyofanyika mjini Washington kesho Alhamisi na Ijumaa kwa sababu ujumbe wa nchi hiyo haujahitimisha uchunguzi wake na wadau muhimu, hii ikiwa ni kulingana na wizara hiyo ya maji, umwagiliaji na nishati kupitia ukurasa wake wa Facebook. Imesema, tayari wamemuarifu waziri wa fedha wa Marekani kuhusiana na hatua hiyo. Tayari ujumbe wa Sudan umewasili nchini Marekani kwa ajili ya mazungumzo hayo.