1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

England yatinga robo fainali Kombe la Dunia

5 Desemba 2022

England imesonga mbele kwenda hatua ya robo fainali ya kombe la dunia linaloendelea nchini Qatar baada ya kuibamiza timu ya taifa ya Senegal bao 3-0 katika mchezo uliopigwa usiku wa Jumapili.

https://p.dw.com/p/4KTx8
FIFA WM 2022 Katar I Achtelfinale | England vs. Senegal
Picha: Manu Fernandez/AP Photo/picture alliance

Senegal, maarufu kama Simba wa Teranga na mabingwa wa soka barani Afrika mwaka uliopita walizima ndoto za bara hilo kunyakua kikombe cha dunia baada ya kukubali kichapo cha fedheha mbele ya maelfu ya watazamaji kwenye uwanja wa Al Bayt.

Timu ya taifa ya Morocco ndiyo wawakilishi pekee wa Afrika waliobakia kwenye michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo ya jana timu ya England itapambana na Ufaransa katika mchezo wa robo fainali baada ya timu hiyo kusonga mble kwa kuifunga Poland bao 3-1. Michezo mingine ya hatua ya mtoano itaendelea leo kwa mchezo wa kwanza kati ya Japan dhidi ya Croatia.