1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eneo muhimu la visima vya mafuta kufunguliwa tena Libya

Sekione Kitojo
5 Machi 2019

maeneo muhimu ya visima vya mafuta nchini Libya yanatarajiwa kufunguliwa baada ya kutekwa na kundi lenye silaha.

https://p.dw.com/p/3ETYt
Libyen Al-Ghani Ölfeld
Picha: Abudllah Doma/AFP/Getty Images

Moja  kati  ya  maeneo  muhimu  ya  visima  vya  mafuta nchini  Libya yanatarajiwa  kufunguliwa  karibu  miezi mitatu  baada  ya  kutekwa  na  kundi  lenye  silaha.

Shirika  linalomilikiwa  na  serikali  la  mafuta  limesema katika  taarifa jana  kwamba  utoaji  mafuta  katika  eneo  la Al-Sharara  kusini  mwa  Libya  unatarajiwa  kuanza  katika muda  wa  wiki  chache  zijazo.

Tangazo  hilo linafikisha  mwisho, hatua  maalum ya kisheria iliyotangazwa  mwezi  Desemba ambayo ililiondolea  shirika  hilo jukumu  la  kushindwa kutimiza mikataba.

Kuanzisha  utoaji  wa  mafuta  tena  kunafuatia kuondolewa  kwa  makundi  yenye silaha  yanayohusika  na kuzuwia  uzalishaji, shirika  hilo  limesema, hali iliyosababisha  upotevu  wa  dola  bilioni  1.8.