1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

El Nino, sio mabadiliko ya tabianchi, chanzo cha ukame

18 Aprili 2024

Ripoti ya wanasayansi iliyotolewa siku ya Alhamisi (Aprili 18) ilisema hali ya ukame iliyosababisha njaa kwa mamilioni ya watu kote katika eneo la kusini mwa Afrika ilitokana na El Nino na sio mabadiliko ya tabianchi.

https://p.dw.com/p/4ewMg
Malawi |  Bangula
Hali ya ukame nchini Malawi, ambako janga la njaa limetangazwa kutokana na hali ya hewa ya El Nino.Picha: Ashley Cooper/Global Warming Images/picture alliance

Mataifa matatu ya kusini mwa Afrika - Zambia, Zimbabwe na Malawi - yalitangaza janga la kitaifa kutokana na ongezeko la hali ya ukame tangu mwezi Januari na kuzorotesha pakubwa sekta ya kilimo, na kushuhudia vifo vya wanyama na mimea. 

Soma zaidi: Zambia yahitaji msaada kukabiliana na ukame

Akiomba msaada wa karibu dola milioni 900 wiki hii, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia alihusisha ukosefu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa.

Soma zaidi: Zimbabwe yatangaza ukame kuwa janga la kitaifa

Lakini wanasayansi kutoka taasisi inayojihusisha na masuala ya hali ya hewa ya World Weather Attribution (WWA) waligundua kuwa ongezeko la joto duniani halina uhusiano wowote na janga hilo.