El Clasico yanukia katika La Liga | Michezo | DW | 16.12.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

El Clasico yanukia katika La Liga

Huko Uhispania ligi kuu ya nchini humo inaendelea kupamba moto pia ambapo wikendi Real Madrid walikosa fursa ya kuingia katika uongozi wa ligi hiyo baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja.

Haya ni wakati ambapo wapinzani na mahasimu wao Barcelona walitoka sare ya mabao mawili pia na Real Sociedad.

Miamba hawa wawili wa La Liga watakuwa wanakutana hapo Jumatano katika uwanja wa nyumbani wa Barcelona Camp Nou katika mtanange wa El Clasico ambao kwa kawaida haukosi cheche.

Msimu uliopita katika mechi iliyochezwa katika uwanja huo, Real Madrid waliangukia pua kwa kucharazwa magoli matano kwa moja.