1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Martin Fayulu aunda vuguvugu jipya la upinzani

Saleh Mwanamilongo, DW Kinshasa28 Agosti 2019

Vuguvugu jipla la kisiasa ambalo limeundwa na kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linajumuisha baadhi ya wapinzani akiwemo mshauri wa zamani wa Etienne Tshisekedi.

https://p.dw.com/p/3Occi
DR Kongo Martin Fayulu
Picha: Getty Images/AFP/T. Charlier

Mgombea alieshindwa kwenye uchaguzi wa rais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Martin Fayulu ameunda vuguvugu jipya la upinzani kwa ajili yakile anachoita kuwa ni kudai maslahi ya wananchi na matokeo sahihi ya uchaguzi. Vuguvugu hilo ambalo linajumuisha baadhi ya wapinzani akiwemo mshauri wa zamani wa Etienne Tshisekedi, linaelezea kwamba Kabila bado anaushawishi mkubwa katika uongozi wa Kongo.

Martin fayulu amesema kwamba serikali mpya iliondwa ni aibu kubwa kwa raia wa Kongo waliotarajia mageuzi. Huku akisema kwamba raia hawana haja ya serikali hiyo bali kukamilisha mahijati yake, huku akimunyoshea kidole cha lawama rais mustaafu Joseph kabila.

"Ni Kabila ndie ana miliki bunge, ni Kabila ndie anamiliki magavana na mabunge za majimbo.Ni Kabila ndie aliteuwa waziri mkuu, ni kabila ambae ana asilimia 65 ya mawaziri kwenye serikali hii mpya. Hiyo ni kuwakejeli raia ambao walipiga kura kwa ajili ya mabadiliko."

Martin Fayulu alikuwa miongoni mwa wagombea wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita. Alikuwa wa pili baada ya Rais Felix Tshisekedi. hata hivyo hakukubaliana na matokeo
Martin Fayulu alikuwa miongoni mwa wagombea wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita. Alikuwa wa pili baada ya Rais Felix Tshisekedi. hata hivyo hakukubaliana na matokeo

Kiongozi huyo wa upinzani ameyasema hayo wakati alipotangaza kuundwa kwa vuguvugu jipya liitwalo Dynamique pour la Verite des Urnes ( DVU). Kwenye vuguvugu hilo wametarajia kuendesha upinzani mkali kwa ajili ya mageuzi nchini DRC,alisema Fayulu.

Miongoni mwa wapinzani waliojiunga na vuguvugu hilo jipya ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Adolphe Muzito, Jeanbaptiste Sonji waziri wa zamani wa afya chini ya utawala wa Laurent Desire Kabila, na Valentin Mubake,moja wapo ya vigogo wa zamani wa UDPS na mtu wa karibu wa hayati Etienne Tshisekedi.

Mubake ambae amempinga rais wa sasa Felix Tshisekedi amesema kwamba uchaguzi uliopita haukuleta mageuzi :

Juhudi za DW kupata maoni kutoka vyama tawala vya CASH na FCC hazikufua dafu.

Mnamo Jumatatu wiki hii, Rais Tshisekedi alitangaza baraza lake la mawaziri ambalo lina mawaziri 66 wengi wao hawajawahi kufanya kazi katika serikali.