1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yatoka nyuma na kuilaza Leverkusen

30 Septemba 2018

Borussia Dortmund ilitoka nyuma mabao mawili kwa sifuri na kuilaza Bayer Leverkusen mabao manne kwa mawili. Dortmund sasa ndio timu pekee katika Bundesliga ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

https://p.dw.com/p/35iqd
Bundesliga Bayer Leverkusen - Borussia Dortmund | Jubel Reus
Picha: Getty Images/Bongarts/L. Baron

Ushindi huo umewaweka vijana hao wa kocha Lucien Favre kileleni mwa msimamo wa ligi na pointi 14 moja mbele ya Bayern Munich ambao walipewa kichapo cha kwanza msimu huu cha mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Hertha Berlin. Schalke ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuifunga Mainz bao moja kwa sifuri.

VfB Stuttgart pia walipata ushindi wao wa kwanza wa msimu kwa kuifunga Werder Bremen mabao mawili kwa moja.

Borussia Moenchengladbach walipanda hadi nafasi ya nne licha ya kutekwa kwa sare ya mabao mawili kwa mawili nyumbani kwa Wolfsburg, ambako hawajawahi kushinda kwa miaka 15.

Werder ambao hawakuwa wamepoteza mchezo wowote kabla ya Jumamosi, wako katika nafasi ya tano na pointi 11 wakati Stuttgart wamepanda hadi 15. RB Leipzig wako nafasi ya sita pia na pointi 11 baada ya kuwafunga Hoffenheim mabao mawili kwa moja.

Nuremberg ilishinda mpambano wa timu zilizopandishwa daraja msimu uliopita wakati ilipoitandika Fortuna Duesseldorf tatu bila.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri. Grace Kabogo