1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dau la Barca laenda mrama

25 Aprili 2022

Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez amewaambia wachezaji wake kwamba wajizatiti ili waweze kumaliza ligi katika nafasi ya pili.

https://p.dw.com/p/4APqx
Spanien Xavi neuer Trainer von Barcelona
Picha: Marc Gonzalez Aloma/Action Plus/imago images

Hii ni baada ya miamba hao ambao walikuwa wamezoea kumaliza msimu katika nafasi ya kwanza kulazwa moja bila na Rayo Vallecano uwanjani Camp Nou hapo Jumapili.

Hii ni mara ya kwanza kwa Barca kupoteza mechi tatu mfululizo nyumbani kwao na kushindwa huku kumetoa nafasi kwa mahasimu wao Real Madrid kuunyakua ubingwa wa La Liga.

Madrid sasa wanahitaji pointi moja tu katika mechi zao tano zilizosalia na Barcelona wana pointi 63 sawa na Sevilla. Mapema mwezi huu Barcelona walibanduliwa kutoka kwenye mashindano ya Europa League na Eintracht Frankfurt.