Dani Alves ″autafuna″ ubaguzi wa rangi | Michezo | DW | 28.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dani Alves "autafuna" ubaguzi wa rangi

Matukio kadhaa ya ubaguzi wa rangi michezoni yanaendelea kushuhudiwa na kuripotiwa katika maeneo mbalimbali duniani, na tukio la karibuni kabisa limemhusu mchezaji Barcelona Mbrazil Dani Alves.

Beki huyo wa Barca aliwajibu mashabiki waliojarobu kuonyesha tendo la kibaguzi wakati akijiandaa kupiga mkwaju wa kona wakati wa ushindi wa timu yake wa mabao matatu kwa mawili nyumbani kwa Villareal.

Alves aliliokota kwa urahisi ndizi lililorushwa uwanjani kutoka upande wa mashabiki, akalitoa maganda na akalitumbukiza mdomoni mwake mara moja kabla yakuyatupa maganda na kuuchanja mwkaju wa kona.

Siyo mara ya kwanza ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil amewahi kujikuta katika hali hiyo. Mwaka jana, Alves mwenye umri wa miaka 30 alilalamika kwa kufanyiwa tendo la kibaguzi baada ya baadhi ya mashabiki kuigizia milio ya nyani wakati wa nusu fainali ya Kombe la Mfalme nyumbani kwa Real Madrid. Na hadi kufikia sasa, hatua hiyo ya Alves kula ndizi, imesifiwa sana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari Uhispania na kwingineko duniani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman