​​​​​​​CR7, Salah, au Modric? | Michezo | DW | 03.09.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

​​​​​​​CR7, Salah, au Modric?

Cristiano Ronaldo anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid Luka Modric na Mmisri Mohammed Salah kuwania tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka wa kwa mara ya sita.

Ronaldo alikuwa mfungaji wa mabao mengi wakati Real Madrid ikinyanyua kombe la Mabingwa Ulaya kwa mara ya nne mfululizo kabla ya kuihama klabu hiyo na kujiunga na Juventus.

Modric pia alikuwa sehemu ya Rwal ambayo ilitawala Champions League katika miaka ya karibuni na kushinda tuzo ya mchezaji bora katika Kombe la Dunia kwa kuifikisha Croatia katika fainali.

Salah alifunga mabao 44 katika msimu wake wa kwanza na Liverpool na pia akafika katika fainali ya Champions League na Liverpool. Lionel Messi amewachwa nje ya orodha hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2006.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef