1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CR7 akasirishwa na swali la mwandishi wa habari

17 Februari 2016

Mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo aliondoka kwa hasira katika kikao cha waandishi wa habari baada ya kuulizwa suali juu ya rekodi ya ufungaji magoli katika mechi za ugenini msimu huu

https://p.dw.com/p/1HwWq
Fußball - Real Madrid CF - FC Barcelona - Clasico
Picha: Getty Images/AFP/J. Soriano

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, amefunga magoli 32 msimu huu lakini hajafunga katika michuano ya ugenini tangu mwezi Novemba.

Alipoulizwa, mbona hali iko ivyo, alijibu "Nani mwingine amefunga magoli mengi ugenini kuliko mimi tangu nimekuja Uhispania? Aliuliza Ronaldo mfungaji namba moja wa Championzi Ligi "Nitajie mchezaji mmoja ambaye amefunga magoli mengi kuliko mimi. Hakuna jibu? Sawa. Asante" Akaondoka. Ronaldo alikuwa akiongea na wanahabari kabla ya mechi ya Real Madrid dhidi ya Roma katika Stadio Olimpico ya ligi ya mabingwa barani Ulaya - UEFA Champions League.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Daniel Gakuba