Coutinho atua Camp Nou | Michezo | DW | 08.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Coutinho atua Camp Nou

Hatimaye uhamisho wa Philippe Coutinho wa kujiunga na Barcelona umekamilika baada ya mchezejai huyo kutambulishwa rasmi kwa maelefu ya mashabiki uwanjani Nou Camp

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 25 alitia saini mkataba na klabu ya Barecelona akiwa pamoja na rais Josep Maria Bartomeu, kabla ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki.

Liverpool na Barca waliafikiana kuhusu uhamisho wa Coutinho Jumamosi ambaye aligharimu kitita cha euro milioni 160.

"Ningependa kumshukuru rais na kila mtu aliyechangia kufanikisha hili," amesema Coutinho. "Nina furaha sana, ni ndoto ambayo imetimia na natumai kwamba nitafanya kazi yangu vyema uwanjani."

Bartomeu amesema mashabiki wote wa Barca wana furaha kumuona Coutinho katika klabu ya Barcelona. Coutinho alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na ingawa alibainika kwamba ana maumivu ya paja lake la kulia, alikamilisha uhamisho wake.

Barcelona wamesema kiungo huyo wa kati huenda akakaa nje wiki tatu hivi. Sasa kuna uwezekano way eye kucheza mtanange wa watani wa jadi maarufu kama debi ya Catalona dhidi ya Espanyol mnamo tarehe 4 Februari.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Abdulrahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com