1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Colombia yawafukuza mabalozi wa Argentina

28 Machi 2024

Wizara ya mambo ya nje ya Colombia imeamrisha kufukuzwa nchini humo kwa wanadiplomasia wa Argentina, baada ya Rais wa Argentina Javier Milei kumuita Rais wa Colombia Gustavo Petro, "gaidi muuaji."

https://p.dw.com/p/4eDQt
Rais wa Argentina Javier Milei
Rais wa Argentina Javier Milei alimuita Rais wa Colombia Gustavo Petro kuwa ni gaidi muuajiPicha: Natacha Pisarenko/AP Photo

Wizara ya mambo ya nje ya Colombia imeamrisha kufukuzwa nchini humo kwa wanadiplomasia wa Argentina, baada ya Rais wa Argentina Javier Milei kumuita Rais wa Colombia Gustavo Petro, "gaidi muuaji." Katika taarifa, Colombia imesema matamshi hayo ya Milei yameivunja heshima na uamunifu wa Rais Petro ambaye alichaguliwa kidemokrasia.

Soma pia:Colombia yaongoza kwa mauaji ya wanaharakati wa mazingira 

Taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Colombia imezidi kueleza kwamba, ubalozi wa Argentina utafahamishwa kwa njia za kidiplomasia ni maafisa gani binafsi wanaokabiliwa na amri hiyo ya kuondoka nchini humo.

Akiwa na umri wa miaka 17, Rais Petro wa Colombia alijiunga na kundi la wapiganaji la M-19 lililokuwa likihusika katika mapigano katika miaka ya 1970 na 1980, ambapo alikamatwa na kufungwa jela kwa miezi 18 kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria.