1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaChina

China yazibana kampuni za Japan, mvutano ukiongezeka

24 Februari 2026

China imeyachukulia hatua makampuni na taasisi 40 za Japan ikiwashutumu kwa kusaidia mipango ya kuimarisha uwezo wa jeshi la Japan.

https://p.dw.com/p/59Jpy
Marekani | Magari mapya aina ya Subaru yakiwa sokoni
China imechukua hatua kali dhidi ya makampuni 40 ya Japan ambayo imedai yanasaidia jeshi la Japan kujiimarisha. Miongoni mwa kampuni hizo ni ya kuzalisha magari aina ya SubaruPicha: Justin Sullivan/Getty Images

Hatua hii ya leo Jumanne ya Beijing inaashiria kuongezeka kwa mvutano wa miezi kadhaa ulioongezeka baada ya Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi mnamo mwezi Novemba kusema kuwa Tokyo inaweza kutumia jeshi lake ikiwa kutakuwa na shambulizi dhidi ya Taiwan.

Wizara ya Biashara ya China imezizuia taasisi 20 za usafirishaji za Japan, baadhi zikiwa za kampuni ya Mitsubishi na shirika la anga za juu la Japan, ikiangazia suala la usalama wa taifa.

Wizara hiyo aidha imeongeza makampuni mengine 20 inayoendelea kuyafuatilia ni pamoja na ya kutengeneza magari ya Subaru ambayo bidhaa zake zinazosafirishwa nje zitakumbwa na ukaguzi mkali zaidi.