1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaanza mazoezi ya kijeshi

13 Juni 2023

China imeanza mazoezi ya kijeshi katika eneo la bahari ya mashariki mwa nchi hiyo kuelekea Kaskazini mwa kisiwa cha Taiwan.

https://p.dw.com/p/4SVM9
Picha hii iliyochukuliwa 2018, inayoonyesha ndege za kivita za J-15 zilizoshiriki mazoezi ya kijeshi.
China inafanya mazoezi haya ya kijeshi, wakati wanachama wa NATO pia wakifanya mazoezi makubwa kabisa, Ulaya.Picha: AFP

Mazoezi hayo yaliyoanza leo yanajumuisha wanajeshi kufyatua silaha za moto kutoka kwenye meli za kivita katika wakati ambapo Marekani na washirika wake wanafanya pia luteka zao za kijeshi katika eneo la magharibi la bahari ya Pasifiki.

Mamlaka ya usalama wa safari za baharini ya China haikutowa tahadhari yoyote kwa kipindi cha kuanzia asubuhi hadi mchana leo Jumanne katika eneo, la pwani ya mji wa Taizhou kuhusiana na matumizi ya silaha za moto zinazofyatuliwa kutoka meli za kivita.

Mazowezi mengine ya kijeshi ya China katika eneo hilohilo yataendelea hadi jioni ya leo. Kimsingi mazowezi aina hii karibu na kisiwa cha Taiwan mara nyingi huzusha ukosoaji kutoka kwa washirika wa Taiwan na hususan Marekani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW