1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Manowari za China zakatiza ujia wa Bahari wa Taiwan

Lilian Mtono
27 Mei 2023

Wizara ya Ulinzi wa taifa ya Taiwan imesema meli tatu za kivita za China, ambazo ni pamoja na manowari ya kutua ndege zimekatiza kwenye ujia wa Bahari wa Taiwan mapema hii leo.

https://p.dw.com/p/4Rt9z
Agosti 28, 2022, manowari ya kijeshi ya Marekani ikiwa katika ujiwa wa bahari wa Taiwan katika operesheni za kawaida za kijeshi.
Marekani na mataifa ya magharibi yanahofia kitisho cha China kuelekea Taiwan. China inadai Taiwan ni sehemu ya himaya yake.Picha: Justin Stack/AFP

Taarifa ya wizara hiyo ya ulinzi wa taifa ya Taiwan, imesema imeziona meli hizo tatu zikiongozwa na manowari hiyo ya Shangdong zikipita kwenye ujia huo wa Taiwan mchana huu na msafara huo ulikuwa ukielekea kwenye mpaka usio rasmi wa bahari unaotenganisha kisiwa hicho na bara la Asia.

Hili ni tukio la karibuni zaidi la China kuonyesha nguvu zake na inalifanya zaidi ya mwezi mmoja baada ya kufanya luteka za kijeshi za angani na majini kukizunguka kisiwa hicho.

China kuwa Taiwan ni sehemu ya himaya yake na imekwishaapa kukichukua kwa kutumia nguvu kama watalazimika kufanya hivyo.