Changamoto baada ya uchaguzi wa Ujerumani | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.09.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Changamoto baada ya uchaguzi wa Ujerumani

Wajerumani wanasubiri kujuwa nani atakayewaongoza .Yeyote atakayeibuka mshindi baada ya uchaguzi mkuu wa leo (22.09.2013) atakabiliwa na changamoto nzito katika kipindi chake cha utawala miaka minne ijayo.

Yeyote atakaeshinda uchaguzi wa Septemba 22, anasubiriwa na mtihani mkubwa

Yeyote atakaeshinda uchaguzi wa Septemba 22, anasubiriwa na mtihani mkubwa

Uchaguzi hutanguliwa na kampeni ya uchaguzi wenyewe na wakati huo siasa hutawala. Lakini hakuna kubwa linalofanyika kwani maamuzi muhimu hubakia miezi kadhaa bila ya kutelezwa. Ukweli huu pia uko kwenye masuala muhimu katika sera ya mambo ya nchi za nje ambapo mnamo majuma machache yaliyopita, hali ilikuwa kimya. Serikali itakayokuwa madarakani baada ya uchaguzi huu mkuu itakabiliwa na changamoto kwa miaka miaka minne ijayo.

Je mgogoro wa sarafu ya euro umefikia wapi?

Bila shaka kitu kimoja ni wazi: Msukosuko wa euro umetulia kidogo tu, huenda ukagonga tena vichwa vya habari karibuni baada ya uchaguzi. Ingawa baadhi ya nchi za Ulaya zinafanya vizuri baada ya msukosuko huo, lakini Ugiriki haiwezi kujikwamua peke yake kwani deni lake la euro bilioni 300 ni kubwa mno.

Angela Merkel wa CDU ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena

Angela Merkel ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa tena

Hata waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble, kutoka chama cha Christian Democratic Union,CDU, ameuambia umma kupitia bunge, Bundestag, kwamba patalazimika paweko mpango mwengine tena wa kuisaidia Ugiriki.

Taasisi maarufu za utafiti wa masuala ya uchumi zinatarajia kwamba mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yatakutana mwishoni mwa mwaka kuamua juu ya msaada mpya, ukiwa ni mzigo mkubwa kwa serikali mpya ya Shirikisho nchini Ujerumani.

Deni la Bajeti ya Ujerumani: Kuweka akiba au afadhali kuamua kutoa zawadi?

Ujerumani kwa hakika iko katika hali bora kuliko nchi nyingi nyingine za Ulaya, uchumi unakuwa na mapato ya kodi ya juu kuliko ilivyowahi kuwa. Pamoja na hayo, serikali ya Ujerumani ina deni la euro trilioni 2.1 na deni linaongezeka kila mwaka kuliko pato lake. Mikoa kadhaa ina mzigo mkubwa wa madeni na serikali nyingi za miji na mitaa ni muflisi. Takriban kila chama kinataka kuibadili hali hiyo .

Mgombea wa chama cha SPD Peer Steinbrück. Wafuasi wake bado wanayo imani

Mgombea wa chama cha SPD Peer Steinbrück. Wafuasi wake bado wanayo imani

Vipi kuibadili hali hiyo: kuweka akiba zaidi au kuongeza kodi? Chama cha Social Democratic, SPD, na chama cha Kijani, alau vimetangaza vinataka wenye pato kubwa walipe kodi ya juu, hilo halikubaliwi na vyama vya CDU na FDP. Angela Merkel alisema wakati wa mjadala wa televisheni dhidi ya mpinzani wake Peer Steinbruck "Mipango ya kuongeza kodi ya Social Democratic na Kijani (Grüne) itazorotesha hali bora ilioko hivi sasa."

Wakati huo huo, vyama vingi vinataka kutumia fedha nyingi kwa miradi wanayoipendelea. Kwa mfano CDU inataka malipo ya juu ya uzeeni kwa akina mama, SPD na Kijani, matumizi zaidi kwa elimu na huduma za watoto. Kwa hiyo Ujerumani italazimika kuwa na mpaka katika ongezeko la deni lake na hadi 2020 lazima iyaweke mambo sawa.

Haki zaidi lakini vipi?

Suala la haki litachukua nafasi kubwa baada ya uchaguzi. Hapa kuna mambo kadhaa. Usoni kabisa ni usawa katika elimu: Kila mtoto anapaswa kuwa na nafasi sawa katika maisha. Kwa wakati huu sivyo ilivyo nchini Ujerumani. Mtoto anayetoka familia ya wasomi na nafasi kubwa zaidi ya kupata elimu na kumaliza kidato cha sita kuliko anayetoka familia ya wasiosoma. Pia suala la usawa wa malipo katika ajira liko usoni katika orodha. “Kuna wengi wanaofanya kazi siku nzima lakini kwa malipo madogo kiasi ya hata kushindwa kukidhi mahitaji yao,” amesema mgombea ukansela wa chama cha SPD, Steinbruck. Kwa hiyo swali ni je, panapaswa kuweko mshahara wa wastani kwa wote nchini Ujerumani?

Mwandishi: Jeanette,Seiffert/Mohammed Abdul-Rahman

Mhariri, Gakuba, Daniel

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com