CDU, SPD zapata ushindi, AfD yajiimarisha zaidi uchaguzi wa majimbo | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.09.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

CDU, SPD zapata ushindi, AfD yajiimarisha zaidi uchaguzi wa majimbo

Matokeo ya chaguzi mbili zilizofanyika Jumapili katika majimbo ya Ujerumani ya Saxony na Brandenburg, yanaonyesha kuwa vyama vya SPD na CDU vimepata ushindi na hivyo kusalia kileleni, licha ya umaarufu wake kupungua.

Chama cha Kansela Angela Merkel cha Christian Democrats CDU kimesalia kuwa chama chenye nguvu kwenye jimbo la Saxony kwa kuibuka na asilimia 32 ya kura. SPD imeendelea kuwa juu katika jimbo la Brandenburg kwa kujinyakulia asilimia 26.2 ya kura, ingawa imeporomoka toka asilimia 31.9 ya uchaguzi uliopita. Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, chama mbadala kwa Ujerumani AfD kimeibuka nafasi ya pili katika majimbo yote mawili na hivyo kujiimarisha zaidi. Chama hicho cha AfD kimetumia hasira ya wapiga kura kuhusiana na sera ya wahamiaji kuweza kujiimarisha zaidi katika eneo hilo la Ujerumani Mashariki ya zamani.

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com