BVB yapata ushindi, Leverkusen yashikiliwa | Michezo | DW | 19.10.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

BVB yapata ushindi, Leverkusen yashikiliwa

Borussia Dortmund ilipata ushindi muhimu katika Champions League nchini Ureno, wakati Leverkusen ilitekwa na Tottenham. Real Madrid ilipata ushindi mnono wakati pia Leicester ikishinda

Sporting Lisbon 1-2 Borussia Dortmund
(Cesar 67‘ - Aubameyang 9‘, Weigl 43')

Julian Weigl alifunga bao safu – lake la kwanza katika kandanda la kulipwa – wakati Borussia Dortmund ilishikilia ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Sporting Lisbon. Dortmund ilichukua uongozi wa mapema kupitia bao safi la Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye alifunga mpira kwa mvisha kanzu kipa Rui Patricio. Elias nusra aisawazishie Sporting wakati alimkwepa beki Matthias Ginter na kuelekea langoni kabla ya kipa kuupangua.

Kisha Coates akavurumisha kitu wavuni bao lakini likafutwa baada ya mshambuliaji wa Sporting Bas Dost kumfanyia madhambi kipa Bürki ijapokuwa picha za televisheni zilionyesha kuwa ulikuwa uamuzi wa utata.

Dortmund walifunga tena dhidi ya wenyeji kabla ya Bruno Cesear kuwafungia Sporting bao la kufutia machozi kutokana na mkwaju wa free kick

Leverkusen na Tottenham zilitoka sare tasa

Leverkusen na Tottenham zilitoka sare tasa

Bayer Leverkusen 0-0 Tottenham Hotspur

Mlinda lango wa Tottenham Hugo Lloris alifany akazi safi sana langoni kwa kuokoa mabao yaliyoinyima Bayer Leverkusen ushindi uwanajni Bay Arena.

Wakati Monaco wakitishia kuponyoka na uongozi wa Kundi E, Leverkusen na Spurs huenda wakajikuta wakipigania nafasi ya pili katika kundi hilo – ma timu zote mbii zilikuwa na nafasi za kupata ushindi jana usiku.

Matokeo ya Champions League:

CSKA Moscow 1-1 Monaco

Leicester 1-0 Copenhagen

Brugge 1-2 Porto

Dinamo Zagreb 0-1 Sevilla

Real Madrid 5-1 Legia Warsaw

Lyon 0-1 Juventus

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Daniel Gakuba