1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi: Mwaka mmoja baada ya Uchaguzi

Amida Issa21 Julai 2016

Leo Julai 21 ni mwaka mmoja tangu Pierre Nkurunziza alipochaguliwa tena kuiongoza Burundi kwa kipindi cha miaka 5, licha ya upinzani kukosowa na kudai ya kuwa katiba ya Burundi haikumruhusu kuwania muhula wa tatu.

https://p.dw.com/p/1JT2i
Burundi Präsident Pierre Nkurunziza
Picha: picture-alliance/dpa/C. Karaba

Utata huo ulisababisha maandamano ya kupinga azma yake, na mauwaji ambayo Umoja wa Mataifa unakadiria yameuwa watu zaidi ya 500. Licha ya usalama kuonekana kurejea hatua kwa hatua kiuchumi nchi inaelezewa kuwa katika hali ngumu kufuatia hatua ya wafadhili wakuu kusitisha misaada ya kifedha. Changamoto kubwa zaidi hata hivyo ni kutopigwa hatua yoyote katika majadiliano ya kisiasa yenye lengo la kumaliza mzozo unaoikabili nchi hiyo kwa mwaka mmoja sasa.

Mwaka mmoja tangu kufanyika uchaguzi Rais Pierre Nkurunziza na serikali yake wameonekana kuimarika kitaifa. Waziri wa usalama Alain Guillaume Bunyoni amesema wamefaanikiwa kupiga hatua kubwa kwa kukabiliana na walokuwa wakiyumbisha usalama.

"Makundi yaliyokuwa yakiendesha uhalifu, silaha zilikuwa zinamilikiwa kinyume na sheria zimeshikwa na mamlaka ya polisi. Na bunduki za aina nyingi zaidi ya 164,guruneti 199, na mabomu kadhaa vimekamatwa, magaidi 35 walijisalimisha mamlaka za usalama" amesema waziri Bunyoni.

Hali ikoje sasa?

Licha ya hatua hiyo, mauwaji yakuvizia bado yame shuhudiwa, tarehe 13 mwezi huu aliuwawa mchana kweupe Mbunge Hafsa Mossi zamani muandishi wa habari, mwenye umaarufu kitaifa ,kikanda na kimataifa. Hadi sasa sababu za kuuwawa kwake bado zimesalia gizani.

Halmashauri ya Umoja wa mataifa inayo husika na haki za binaadamu imekadiria kuuwawa kwa watu zaidi ya 500 katika kipindi cha mwaka huu mmoja.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Nyamitwe
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain NyamitwePicha: DW/A. Issa

Wakati serikali ikionekana kuweka nguvu katika kurejesha usalama, raia walalamika kuumia kiuchumi ambapo faranga ya Burundi yashuhudiwa kuporomoka thamani ukilinganisha na pesa ya kigeni. Baadhi ya wananchi wa mjini Bujumbura wanasema kuwa maisha yamezidi kuwa magumu hasa katika masoko kwa kuwa bidhaa zinapanda bei. Hii ni baada ya wahisani wakuu kusimamisha misaada ya kifedha.kamwe serikali haitoketi kwenye meza moja ya majadiliano na walohusika na jaribio la kutaka kuipindua serikali kwa sababu kwa kufanya hivyo itakuwa ni kupinga misimamo mbalimbali.

Mazungumzo ya amani

Baada ya vikao kadha kufanyika Arusha tangu kuteuliwa Benjamin Mkapa rais Mustaafu wa Tanzania kuwa mpatanishi bado serikali ya Burundi kupitia waziri wa mambo ya nje Alain-Aime Nyamitwe amekumbusha kuwa kamwe serikali haitoketi kwenye meza moja ya majadiliano na walohusika na jaribio la kutaka kuipindua serikali kwa sababu kwa kufanya hivyo itakuwa ni kupinga misimamo mbalimbali. Wahisani wameweka kigezo kikuu ni kupiga hatua kwenye majadiliano jumuishi yenye dhamira ya kumaliza mzozo huo ulozuka leo mwaka mmoja. Matarajio ya raia wa Burundi ni kuona mgogoro huo unatafutiwa jawabu kwa wanasiasa wote kuketi chini na kumaliza tofauti zao ili amani iweze kurejea.