1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani laidhinisha sheria ya kurahisisha uraia

Grace Kabogo
19 Januari 2024

Wabunge wa Ujerumani Ijumaa wamepiga kura kuidhinisha sheria ambayo itarahisisha mchakato kwa wahamiaji kupata uraia wa nchi mbili.

https://p.dw.com/p/4bTCP
Ujerumani I Bunge
Bunge la Ujerumani limeridhia sheria itakayoruhusu uraia wa nchi mbili yenye lengo la kuvutia zaidi wafanyakazi kutoka mataifa menginePicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Serikali ya Ujerumani inasema sheria hiyo inapaswa kusaidia kuifanya Ujerumani kuwavutia zaidi wafanyakazi wenye ujuzi kimataifa na kusaidia kupunguza uhaba wa wafanyakazi.

Wabunge 382 wamepiga kura ya ndiyo na 234 hapana, huku wabunge 23 wakijizuia kupiga kura. Chini ya sheria mpya, raia wa kigeni wataweza kuomba uraia wa Ujerumani baada ya kuishi miaka mitano badala ya miaka minane.

Kwenye mazingira ambayo muombaji ametengamana vizuri na jamii, atakuwa na uwezo wa kupata uraia baada ya miaka mitatu.

Uraia wa nchi mbili kwa kawaida unaruhusiwa tu kwa raia wa nchi za Umoja wa Ulaya au Uswisi. Vyama vya upinzani vya kihafidhina ambavyo vinapinga sheria mpya vinataka mabadiliko ambayo yatalinda thamani ya uraia wa Ujerumani.