Brazil yafuzu hatua ya mtoano ya 32 bora Kombe la Dunia
25 Juni 2026
Ushindi huo umeihakikishia Brazil nafasi ya kwanza kwenye kundi hilo, ikiwapiku Morocco kwa tofauti ya mabao, baada ya Morocco kushinda 4–2 dhidi ya Haiti mjini Atlanta.
Katika ushindi huo, mashabiki wa Brazil walipata habari njema baada ya Neymar, mshambuliaji mkongwe na mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo, kurejea uwanjani kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo, akiingia katika kipindi cha pili na kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.
Katika Kundi A, Afrika Kusini pia imefuzu hatua ya mtoano baada ya kuichapa Korea Kusini bao 1–0 mjini Monterrey na kumaliza katika nafasi ya pili.
Bafana Bafana sasa watakutana na Canada, ambao wameandika historia kwa kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza licha ya kupoteza 2–1 dhidi ya Uswisi mjini Vancouver.