1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia Moenchengladbach yajizatiti kileleni mwa Bundesliga

Sekione Kitojo
2 Desemba 2019

Borussia Moenchengladbach haijabahatisha kukaa kileleni mwa ligi ya Ujerumani Bundesliga, Kocha  mpya Bayern Munich  aonja  kipigo, wakati Juergen Klinsmann nae aanza kwa kipigo akiwa kama kocha wa Hertha BSC Berlin.

https://p.dw.com/p/3U6Bp
Fußball Bundesliga SC Freiburg - Borussia Mönchengladbach
Picha: picture-alliance/U. Hufnagel

Viongozi wa  ligi Borussia Moenchengladbach  tayari  wameonesha mshangao wa  kupanda hadi  kileleni  mwa  msimamo wa  ligi  kuwa si kwa  bahati  mbaya  na ushindi  wao  jana  wa  mabao 4-2  dhidi  ya  Freiburg  inaleta  mvuto katika  pambano  la  siku  ya  Jumamosi  dhidi ya  mabingwa watetezi  Bayern Munich , ambayo  siku  ya  Jumamosi  ilichezea kipigo cha  mabo 2-1  dhidi  ya  Bayer Leverkusen nyumbani. Gladbach , ambayo  imeshinda  michezo  minane  katika  michezo yao 10  iliyopita, imefungua  mwanya  wa  pointi 4 mbele  ya  Bayern Munich  iliyoko  katika  nafasi ya  4 na wanashika  usukani wa  ligi kwa  wiki  ya  saba  mfululizo, ikiwa  ni mwendo wao  bora  kabisa tangu  msimu  wa  mwaka  1977  ambapo  walinyakua  taji  hilo la Bundesliga.

Fußball Bundesliga SC Freiburg - Borussia Mönchengladbach
Mshambulia raia wa Uswisi Breel Embolo akipongezwa na wachezaji wenzake Marcus Thuram, na patrick Herrmann na Laszlo Benes baada ya kupachika bao.Picha: Getty Images/AFP/I. Fassbender

Huyu  hapa  mlinzi  wa  Bayern Munich  Joshua Kimmich akizungumzia  kipigo  cha  kwanza  tangu  timu  hiyo  kumtimua kocha  wake  mkuu  Niko Kovac ilipokutana  na dhidi  ya  Gladbach siku  ya  Jumamosi  jioni.

"Idadi  kubwa  ya  nafasi za  kupata  mabao ilikuwa  kwetu, tangu wakati ambao  naweza  kuukumbuka, hakuna wakati tulikuwa  na nafasi  kama  hizo kupata  mabao. Pia  tumekuwa  katika  hali  ya kuotea  mara  mbili  au  tatu, lakini  pamoja  na  hayo, takriban tulistahili  kuwa  sare ya  2-2 tukienda  mapumziko. Na  hata  baada ya  kuanza kipindi cha  pili tulipata  pia  nafasi mbili  ama  tatu  za kupata  mabao."

1. Bundesliga | Bayern Munich vs Bayer Leverkusen | Enttäuschung (1:2)
Wachezaji wa Bayern Thomas Mueller (kulia) na Goretzka wakiwa wameduwaa bila kujua kilichotokea baada ya kipigo dhidi ya LeverkusenPicha: Reuters/A. Gebert

Baada  ya  kushinda  mara  nne  bila  nyavu  zao  kutikiswa chini  ya kocha  wa  mpito  Hansi Flick, Bayern ilirejeshwa  kutoka  uwingu wa juu  kwa  kipigo  hicho, nyumbani dhidi ya  Leverkusen.

Kocha  wa  zamani wa  timu  ya  taifa  ya  Ujerumani  Juergen Klinsmann amerejea  katika  ukufunzi  wa   timu  za  Bundesliga baada  ya  kuondoka  muongo mmoja  uliopita lakini kazi  hiyo  akiwa na  Hertha Berlin ilitiwa  doa  na  kipigo cha  mabao 2-1  nyumbani dhidi  ya  makamu  bingwa  wa  Bundesliga  Borussia  Dortmund. "Tulihitaji  zaidi kidogo. Hatutaongeza nguvu  zaidi,"  amesema Klinsmann, ambaye  pia  ni mjumbe  wa  bodi  ya  klabu  hiyo.

Fußball Bundesliga Bayern München - Bayer Leverkusen | Jubel TOR Leverkusen, Leon Bailey
Leon Bailey muuaji wa Bayern MunichPicha: picture-alliance/dpa/M. Balk

"Walikuwa wamejikusanya  mno nyuma na  kimsingi  walipaki basi, na  kuweza  kupenya  kuelekea golini, unahitaji washambuliaji watano. Hii  ni  vigumu  sana. Lakini  jinsi timu  ilivyocheza, kujituma, kama  walivyokuwa wakisaidiana, pia kukimbia  sana na mapambano ya mtu  na  mtu, ilikuwa  vizuri sana. Kutokana  na  hayo tunapaswa kujenga , na tumefanya  hivyo kwa  kazi  kubwa na  kujenga  tabaka la  mafanikio, ambalo  hatimaye  pointi zitakuja."

Kocha  wa  Borussia  Dortmund  ambaye amekabiliwa  na  ukosoaji mkubwa  wa  kikosi  chake  kukosa msisimko uwanjani , amepumua kidogo  kutokana  na  ushindi  huo, baada  ya  vipigo  na  sare ambazo zilisababisha mashabiki na  wachambuzi  wa  masuala  ya kandanda  nchini  Ujerumani kutak  viongozi  wa  klabu  hiyo wamtimue kocha  huyo Mswisi Lucien Favre. Borussia  Dortmund mara  nyingi imekuwa  ikionesha  mchezo mzuri kwa  dakika  chache uwanjani  na  kisha  kupoteana  na  kusababisha  maadui kupenya ngome  yao  kirahisi. Baada  ya  pambano  hilo alisema.

Fußball Bundesliga | Hertha BSC vs. Borussia Dortmund
Mchezaji wa kiungo wa Borussia Dortmund Axel Witsel akichanja mbuga akimtoka mchezaji wa Hertha Berlin, Dodi Lukebakio (kushoto) Picha: Getty Images/AFP/O. Andersen

"Tunapaswa  kuendelea  kupambana  kama  hivi. Tumejilinda  vizuri, tumekimbia  sana. Ilikuwa ni kikosi  kimoja cha  timu."

FC Kolon ilifanikiwa  kwa  mara  ya  kwanza  katika  muda  wa  wiki 4 zilizopita kupoteza  pointi, baada  ya  kutoka  sare ya  bao 1-1  na FC Augsburg ikiwa  na  kocha  wake  mpya  Markus Gisdol katika mchezo  wa  pili  tangu  ashike  madaraka. Gisdol alisema  baada  ya mchezo  dhidi  ya  Augsburg:

"Awali ya  yote juhudi tuliyoweka  katika  mchezo, hasa  katika kipindi  cha  pili, imeturidhisha. Tulipambana , kama  nilivyokuwa nikitarajia. Tuliungwa  mkono  pia  na  mashabiki wetu. na  baada  ya hapo ilikuwa  tu  swali  na  muda , hadi  kupata  bao. Tungeweza  pia kubadili  matokeo  ya  mchezo  huo. Lakini  tunaridhika na pointi moja, na  kwamba  tumeweza  kurejea  katika  mchezo."

Leo jioni mchezo wa  13  wa  Bundesliga utakamilika , kwa  mchezo kati ya  FC Mainz 05  ikiikaribisha  Eintracht Frankfurt.