Borussia Dortmund wafikiria kumsajili Anthony Martial | Michezo | DW | 29.09.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Borussia Dortmund wafikiria kumsajili Anthony Martial

Klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Anthony Martial, 25.

Klabu hiyo  ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga imesema leo Jumatano kwamba itamkosa kiungo wake Mahmoud Dahoud kwa sasa. Mchezaji "aliweka kano kwenye goti lake la kushoto" wakati wa Mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya klabu ya Sporting Lisbon Jumanne, taarifa imesema Dahoud alilemaza uwanja baada ya dakika mbili tu kucheza na nafasi yake ikachukuliwa na Julian Brandt. 

Dahoud alikuwa tayari ametolewa nje ya mechi ya Bundesliga dhidi Augsburg Jumamosi kwa sababu alipokea kadi nyekundu dhidi ya Borussia Moenchengladbach wikendi iliyopita.

Soma pia: Messi ni mchezaji rasmi wa PSG sasa

Wachezaji wa klabu ya BOrussia Dortmund kwenye mechi dhidi ya Sporting Lisbon

Wachezaji wa klabu ya BOrussia Dortmund kwenye mechi dhidi ya Sporting Lisbon

Kwingineko ni klabu ya Barcelona ya nchini Uispania wameungana na Bayern Munich katika kinyang'anyiro cha kumsaka winga wa Ajax Mbrazili Antony, 21. Chelsea na Bayern Munich kwa sasa hawana mpango wowote wa kubadilishana wachezaji kati ya winga wa Marekani Christian Pulisic, 23, na winga wa Bayern Mjerumani Leroy Sane,25, licha ya uvumi unaoendelea.

Soam pia:Barcelona yaachwa hoi Champions League, kocha ajitetea

Barcelona wamepokea ofa kutoka kwa kampuni ya Dubai ya kununua deni la klabu hiyo la euro bilioni 1.5

Klabu ya Uingereza ya Tottenham huenda wakasubiri hadi msimu ujao badala ya Januari kabla ya kujaribu kumuuza tena Dele Alli,25, ikizingatiwa thamani ya kiungo huyo wa kati wa England ilivyoshuka.