1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken: Nafasi ya kusitisha mapigano Gaza inapungua

Lilian Mtono
21 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema mianya inapungua katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Israel na Hamas kuhusiana na usitishwaji mwingine wa mapigano na kuachiliwa mateka.

https://p.dw.com/p/4dxph
Saudi Arabia |  Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken anaitembelea Mashariki ya Kati kwa mara ya sita. Picha: Evelyn Hockstein/AP Photo/picture alliance

Marekani, Misri na Qatar kwa wiki kadhaa wamekuwa wakijaribu kuratibu makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza pamoja na kuchiliwa mateka zaidi waliotekwa na Hamas katika shambulizi la Oktoba 7.

Kwenye mahojiano na mtandao wa Al-Hadath ya Saudi Arabia, Blinken amesema mianya inapungua na anaamini kuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano.

Blinken anazuru Mashariki ya Kati kwa mara ya sita sasa tangu kuanza kwa vita hivyo. Amewasili nchini Misri hii leo ambapo atakutana na maafisa mbalimbali wa serikali na kesho ataelekea Israel.