1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken akumbusha "uwajibikaji" kati ya Marekani na China

Lilian Mtono
25 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken hii leo ameitolea wito nchi yake na Marekani kuzikabili tofauti zao "kwa kuzingatia uwajibikaji" wakati akianza ziara yake nchini China.

https://p.dw.com/p/4f9ms
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Antony Blinken awasili China
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili nchini China kwa ziara inayolenga kusuluhisha baadhi ya masuala baina ya mataifa hayoPicha: Mark Schiefelbein/AP//Pool AP/dpa/picture alliance

Blinken amesema mataifa hayo yanawajibika sio tu kwa watu wao bali ulimwengu mzima na kwa maana hiyo wanalazimika kusimamia uhusiano baina yao kwa uwajibikaji. Blinken amesema hayo mjini Shanghai alipokutana na kiongozi wa Chama cha Kikomunisti.

Blinken yuko ziarani China akilenga kusaka suluhu ya masuala kadhaa yanayotishia utulivu wa kimahusiano baina ya mataifa hayo.

Atakutana pia na viongozi wa kibiashara kabla ya kwenda Beijing kesho Ijumaa kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, na pengine atakutana  na Rais Xi Jinping.

Wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu kubwa kiuchumi ulimwenguni yameimarika kwa kiasi fulani tangu ziara yake ya mwezi Juni, ambapo hadi wakati huo alikuwa afisa wa ngazi za juu kabisa wa Marekani kuzuru China baada ya miaka mitano.