1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bingwa wa mbio za marathon Kelvin Kiptum kuzikwa leo Ijumaa

John Juma
23 Februari 2024

Mazishi ya bingwa wa rekodi ya dunia ya mbio za marathoni nchini Kenya Kelvin Kiptum yanafanyika hii leo Ijumaa baada ya mwanariadha huyo aliyekuwa na umri wa miaka 24 kufariki katika ajali ya gari.

https://p.dw.com/p/4cmzr
Mazishi ya kitaifa ya mwanariadha wa Kenya Kelvin Kitpum
Kiputm anafanyiwa mazishi ya kitaifaPicha: Luis Tato/AFP

Rais wa Kenya William Rutona rais wa chama cha riadha Duniani Sebastian Coe, wanatarajiwa kuwa miongoni mwa waombolezaji watakaohudhuria mazishi ya Kiptum.

Kelvin Kiptum atazikwa Naiberi, karibu na mji wa Eldoret magharibi mwa Kenya katika mkoa wa Bonde la Ufa.

Serikali inajenga makazi mapya kwa ajili ya familia ya shujaa huyo wa taifa la Kenya.

Kocha wake raia wa Rwanda Gervais Hakizimana, aliyekuwa na umri wa miaka 36, alifariki pia katika ajali hiyo alizikwa katika mjini Kigali siku ya Jumatano.