1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bila wapinzani mkutano wa Geneva hauwezekani

2 Novemba 2013

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Mataifa ya Kiarabu nchini Syria Lakhdar Brahimi amesema mkutano wa kimataifa wa amani hautawezekana bila ya wapinzani wa Syria, na Umoja wa mataifa ukionya kuhusu ongezeko la utapiamlo.

https://p.dw.com/p/1AATf
International peace envoy for Syria Lakhdar Brahimi speaks to the media after meeting Syrian President Bashar al-Assad in Damascus December 24, 2012. Brahimi met with President Bashar al-Assad in Damascus on Monday to discuss a solution to the country's 21-month-old conflict. Brahimi told journalists after the meeting that he discussed the situation in Syria overall and gave his views on how to solve the crisis. He said conditions in the country were still poor.(R) Syria's Deputy Foreign Minister Faisal al-Miqdad .REUTERS/Khaled al-Hariri (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Lakhdar Brahimi akizungumza na waandishi habariPicha: Reuters

Akitaraji kuendeleza msukumo wa makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita kati ya Marekani na Urusi ya kuharibu hazina ya silaha za sumu nchini Syria ifikapo katikati ya mwaka 2014, mjumbe huyo Lakhdar Brahimi amekuwa akisafiri huku na huko katika eneo hilo kutafuta kuungwa mkono kwa kile kinachojulikana kama mazungumzo ya pili ya Geneva.

Upinzani nchini Syria umekataa kuhudhuria hadi pale suala la kujiuzulu kwa utawala wa rais Bashar al-Assad litakapowekwa katika ajenda, dai ambalo linakataliwa na serikali hiyo. Makundi ya waasi yameonya kuwa kushiriki katika mazungumzo hayo kutaonekana sawa na usaliti.

U.N.-Arab League peace envoy Lakhdar Brahimi addresses the media after a meeting with Russia's Foreign Minister Sergei Lavrov in Moscow October 29, 2012. Brahimi expressed regret on Monday that a U.N.-brokered truce had not been more successful in Syria but said he would not let this discourage his peace efforts. REUTERS/Maxim Shemetov (RUSSIA - Tags: POLITICS HEADSHOT)
Lakhdar BrahimiPicha: Reuters

Mkutano hautawezekana

"iwapo upinzani hautahudhuria hakutakuwa na mkutano wa Geneva," Brahimi amesema mjini Damascus siku ya Ijumaa, kabla ya kusafiri kwenda mjini Beirut. Mwanadiplomasia huyo wa siku nyingi raia wa Algeria amekutana na Assad siku ya Jumatano, na kusema serikali ya Syria imekubali kushiriki katika mazungumzo hayo na kwamba upinzani unajaribu kutafuta njia ya kuwakilishwa."

Source News Feed: EMEA Picture Service ,Germany Picture Service Syria's President Bashar al-Assad (R) meets International peace envoy for Syria Lakhdar Brahimi in Damascus December 24, 2012 in this handout photograph released by Syria's national news agency SANA. Brahimi met with Assad in Damascus on Monday to discuss a solution to the country's 21-month-old conflict. Brahimi told journalists after the meeting that he discussed the situation in Syria overall and gave his views on how to solve the crisis. He said conditions in the country were still poor. REUTERS/Sana (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Lakhdar Brahimi(shoto) na rais Assad(kulia)Picha: Reuters

Mzozo huo uliodumu sasa kwa muda wa miezi 31 pia umesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu. Siku ya Ijumaa (01.11.2013), shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya chakula limeeleza hofu yake juu ya ukosefu mkubwa wa chakula na watoto wakikabiliwa na njaa katika maeneo yaliyozingirwa.

Njaa na utapiamlo

"Shirika la mpango wa chakula duniani linawasi wasi juu ya hatma ya Wasyria wengi ambao wamekwama katika maeneo ya mzozo na bado wanahitaji msaada wa haraka wa chakula," msemaji wa shirika hilo Elisabeth Byrs amewaambia waandishi habari mjini Geneva. "Tunafuatilia ripoti zinazotia hofu zinazotoka miongoni mwa watoto wenye utapiamlo katika maeneo yaliyozingirwa," amesema.

Kuna hali ya ongezeko la idadi ya watoto ambao wanapatiwa matibabu wakiwa na kiwango cha kati na cha juu cha utapia mlo. Wengi wao wamefikishwa katika hospitali mbili za rufaa mjini Damascus," ameongeza msemaji wa shirika la UNICEF Marixie Mercado.

Mamia ya wanawake, watoto na wazee wameondolewa wiki hii kutoka katika mji uliozingirwa wa moadamiyet al-Sham , kusini magharibi ya Damascus.

(130913) -- ISTANBUL, Sept. 13, 2013 () -- President of the Syrian Coalition Ahmad Al-Jarba (C) attends a meeting of the Syrian National Coalition (SNC) in Turkey's Istanbul on Sept. 13, 2013. The SNC, the main opposition umbrella group in exile, convened its general assembly in Istanbul on Friday to elect their interim "prime minister" and to discuss the Russian proposal on Syria. (/Lu Zhe)
Mkutano wa kundi la upinzani la Muungano wa Kitaifa nchini Syria mjini IstanbulPicha: picture alliance/Photoshot

Maeneo mengi mengine bado yamezingirwa na majeshi tiifu kwa rais Assad , na siku ya Ijumaa wilaya nyingi kati ya hizo katika ukanda wa kusini ya Damascus yalishambuliwa kwa makombora, wamesema wanaharakati. Katika nchi jirani ya Lebanon , shirika la Umoja wa mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF , limeripoti siku ya Ijumaa kuwa zaidi ya watoto laki nne ambao ni wakimbizi kutoka Syria wanahitaji haraka msaada , hususan wakati majira ya baridi kali yakikaribia.

"Jumuiya ya kimataifa haiwajibiki tu kutoa misaada ya kiutu kwa watoto lakini pia inawajibu kusaidia juhudi za Lebanon" za kuwasaidia wakimbizi, amesema mkurugenzi wa UNICEF Anthony Lake, ambaye ameitembelea nchi hiyo hivi karibuni.

Wakati huo huo kundi kuu la upinzani la muungano wa kitaifa limesema lina panga kukutana Novemba 9 kuamua iwapo lishiriki katika mazungumzo ya amani ya Geneva, lakini baraza la taifa la Syria , likiwa ni kundi muhimu, limetishia kujitoa iwapo muungano huo utashiriki mazungumzo hayo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani