BERLIN:Ujerumani yathibitisha kutekwa nyara mwananchi wake mwengine Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 19.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Ujerumani yathibitisha kutekwa nyara mwananchi wake mwengine Afghanistan

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imethibitisha kuwa mjerumani mwengine ametekwa nyara nchini Afghanistan.

Mjerumani huyo mwanamke aliekuwa anafanya kazi kwenye shirika la kutoa misaada alitekwa ndani ya mkahawa na watu wanne waliokuwa na silaha.

Msemaji wa shirika hilo la misaada bwana Ulf Baumann pia amehibitisha juu ya kutekwa nyara mama huyo bila ya kutoa maelezo zaidiAmesema anachojua ni kwamba mama huyo alitekwa nyara ndani ya mkahawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com