BEIRUT: Mbunge aliyeuawa Lebanon azikwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Mbunge aliyeuawa Lebanon azikwa.

Mamia ya waombolezaji wamelisindikiza jeneza la mbunge Walid Eido aliyeuawa mjini Beirut jana baada ya shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari.

Lebanon leo imeadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezi kutokana na mauaji ya mbunge huyo aliyekuwa akiipinga Syria.

Walid Eido alifariki dunia pamoja na mwanawe na watu wengine wanane.

Walid Eido, ambaye amezikwa leo, ni miongoni mwa watu kadha wanaoipinga Syria waliouawa nchini Lebanon tangu mwaka 2005 wakati waziri mkuu wa zamani, Rafik al-Hariri alipouawa.

Washirika wa Walid Eido wameishtumu Syria kwa mauaji hayo wakisema ni njama za kuvuruga shughuli za mahakama ya kimataifa ya kuchunguza waliomuua Rafik al-Hariri.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com