Bayern yatoka sare na Man United | Michezo | DW | 02.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern yatoka sare na Man United

Manchester United walionyesha mchezo wa kujituma, ili kutoka sare ya goli moja kwa moja na Bayern Munich katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana usiku

Katika mechi nyingine Atletico Madrid walitoka sare ya goli moja kwa moja nyumbani kwa Barcelona. Bayern walipata faida ya goli la ugenini lililopachikwa wavuni katika dakika ya 67 kupitia kombora la mguu wa kushoto lake Bastian Schweinsteiger, baada ya Nemanja Vidic kutikisa wavu wa Bayern kwa njia ya kichwa safi kutokana na krosi ya kona dakika nane kabla.

Mshambuliaji wa Bayern Arjen Robben alisema mechi hiyo ilikuwa nzuri, licha ya kuwa United walicheza mchezo wa kulikinga lango lao sana na kusubiri tu nafasi za kushambulia. Amesema sare ya bao moja kwa moja ni matokeo mazuri ya kupeleka nyumbani Munich, ambapo wanataraji kumalizia kibarua hicho wiki ijayo. Aliongeza kuwa siyo rahisi wakati mpinzani anapokaa kwenye lango lao na kufunga mianya yote.

David Moyes na Pep Guardiola wamekuwa na misimu ya kwanza tofauti kabisa katika vilabu vyao

David Moyes na Pep Guardiola wamekuwa na misimu ya kwanza tofauti kabisa katika vilabu vyao

Bayern waliudhibiti mpira mchezo mzima lakini United hawakuwapa nafasi za kunusia lango lao, hali iliyomfanya Robben kujaribukusukumakombora la mbali ambalokipawaUnited David de Gea alilipangua. United walikuwa na nafasi nzuri baada ya Danny Welbeck kumpokonya mpira beki wa Bayern Jerome Boateng aliyeteleza lakini maarifa yake ya kuona lango yakazimwa na kipa Manuel Neuer. Hata hivyo mambo hayakumwendea vyema Schweinsteiger baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Wayne Rooney. Javi Martinez pia atakosa mechi ya mkondo wa pili baada ya kukusanya kadi nyingi za njano katika kinyang'anyiro hicho. Mkufunzi waUnited David Moyes amesema vijana wake walicheza vuzuri na hivyo wamefurahishwa na matokeo hayo. Ameongeza kuwa watajaribu kufunga goli la ugenini mjini Munich.

Atletico wapata goli la ugenini

Nchini Uhispania, Atletico Madrid walikuwa wa kwanza kufunga goli wakati Diego alipochukua mpira baada ya mkwaju wa free kick na kuvurumisha wavuni kombora kali katika dakika ya 56. Diego alikuwa ameingia uwanjani kama mchezaji nguvu mpya katika kipindi cha kwanza wakati mshambuliaji nyita Diego Costa alipoondoka uwanjani kwa sababu ya jeraha.

Barcelona hata hivyo walishambulia na wakasawazisha katika dakika ya 71 wakati Neymar alipobusu wavu baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Andres Iniesta. Katika mechi nyingine za leo za robo fainali, Paris St Germain inawaalika Chelsea wakati Borussia Dortmund ikisafiri kucheza na Real Madrid.

Mwandishi. Bruce amani
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman