1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wazivunja tena nyoyo za mashabiki wa Dortmund

31 Mei 2023

Sherehe za taji la 11 mfululizo la ubingwa wa kandanda wa Ujerumani mjini Munich zingali zikiendelea baada ya Bayern Munich kuwalaza FC Cologne katika dakika ya mwisho siku ya Jumamosi na kunyakua ubingwa huo.

https://p.dw.com/p/4RwA6
Fussball Bundesliga, 34. Spieltag l  Bayern München wird Deutscher Meister
Picha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Mshambuliaji wa Bayern Thomas Müller amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa jinsi walivyokuwa na wachezaji hata walipokuwa wakipitia kipindi kigumu.

"Kulikua na sababu za kutuzomea ila nilichosikia kutoka kwenu ni msukumo mliotupa na ninachotaka kusema ni kwamba msukumo huo ulikuwa wenye umuhimu hata kwenye kipindi kigumu ni muhimu kuendelea kujaribu. Tunaweza kuichambua mechi baadae na nafikiri bado kuna mengi tunayostahili kuyafanya ila ni muhimu kuwa pamoja hata matokeo yanapokuwa mabaya," alisema Müller.

Jamal Musiala aliyewafungia Bayern goli la pili na la ushindi alikuwa na haya ya kusema wakati wa sherehe za taji lao.

"Sina maneno ya kuelezea nilivyojihisi ila ulikuwa wakati mzuri na ninafurahi tumeshinda ligi," alisema Musiala.

Fussball Bundesliga, 34. Spieltag l FC Köln vs FC Bayern München l Tor 1:2 Musiala
Jamal Musiala baada ya kufunga goli la ubingwaPicha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Bayern ambao timu yao ya wanawake pia ililishinda taji la Ligi ya wanawake baada ya kuwabwaga Wolfsburg, mara baada ya kulishinda taji hilo, walimuachisha kazi afisa mkuu mtendaji oliver Kahn pamoja na mkurugenzi wa michezo Hassan Salihamidzic. Nafasi ya Kahn sasa imechukuliwa na Jan-Christian Dreesen.