Bayern warudi uongozini mwa Bundesliga | Michezo | DW | 15.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern warudi uongozini mwa Bundesliga

Bayern Munich wamerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga baada ya kuizaba Fortuna Düsseldorf magoli 4-1 katika mechi ya mzunguko wa ishirini na tisa iliyochezwa hapo Jumapili.

Kingsley Coman ndiye aliyekuwa nyota kwenye mpambano huo baada ya kutikisa wavu mara mbili kisha Serge Gnabry na Leon Goretzka wakapata bao moja kila mmoja huku Dusseldorf wakipewa bao lao moja na mshambuliaji Dodi Lukebakio.

Hii ina maana kwamba Bayern sasa wamechukua usukani wa ligi hiyo wakiwa na pointi 67 huku mahasimu wao Borussia Dortmund wakiwa na pointi 66 baada ya kuto ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mainz siku ya Jumamosi ambapo chipukizi Jadon Sancho aliwafungia Dortmund magoli yote mawili.