Bayern Munich yaitandika Salzburg bao 7-1 | Michezo | DW | 09.03.2022
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern Munich yaitandika Salzburg bao 7-1

Robert Lewandowski amevunja rekodi ya kufunga hat-trick ndani ya dakika 11 na kuifanya Bayern Munich kusonga hatua ya robo fainali katika michuano ya Champions League kwa ushindi wa bao 7-1 dhidi ya Red Bull Salzburg .

Mshambuliaji huyo wa Poland alifunga bao tatu kufikia dakika ya 23, ikiwa ni bao za mapema kufungwa na mchezaji yeyote ndani ya michuano ya Champions League.

Nahodha wa Bayern Manuel Neuer alisema kuwa "hiyo bila shaka ilikuwa ni ujumbe kutoka kwetu na inatupa matumaini kuwa kutakuwa na mambo kama hayo".

Mabingwa wa Austria, Salzburg walikuwa wamewabana Bayern kwa sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza, lakini matumaini yao ya kuwika mjini Munich yaliingia doa pale Lewandowski alipofunga bao la kwanza na mikwaju miwili ya penalti kuwapeleka Bayern kwenye njia yao ya kupata ushindi.

Bayern walianza na mashambulizi mazito, lakini walionekana kupwaya nyuma na kulikuwa na nafasi kwenye lango zote mbili dakika za mwanzo.

Liverpool walijiunga na Bayern katika hatua ya robo fainali licha ya Inter Milan kushinda 1-0 kwenye Uwanja wa Anfield.

Siku ya Jumatano Real Madrid watajaribu kupindua  meza baada ya kufungwa 1-0 nyumbani na Paris Saint-Germain na Manchester City atakutana na Lisbon.