Bayern Munich waanza Bundesliga kwa kuchechemea | Michezo | DW | 19.08.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern Munich waanza Bundesliga kwa kuchechemea

Msimu mpya wa Bundesliga uling'oa nanga wikendi iliyokwisha na usiku wa Ijumaa Bayern Munich walianza kwa kuchechemea kwani licha ya kuwa nyumbani walilazimishwa sare ya magoli mawili na Hertha Berlin.

Robert Lewandowski ndiye aliyewafungia Bayern magoli yote la pili akilifunga kupitia mkwaju wa penalti kisha Dodi Lukebakio aliyewafunga Bayern msimu uliopita hapo Allianz Arena wakati akiichezea Fortuna Düsseldorf, safari akafunga goli la kwanza la Hertha.

Marko Grujic ndiye aliyefunga bao la pili baada ya mchezo mzuri kutoka kwa Hertha Berlin.

Jumamosi Borussia Dortmund wakawaduwaza Augsburg magoli matano kwa moja uwanjani Signal Iduna Park.

Bundesliga | 1. Spieltag | Borussia Dortmund - FC Augsburg (Reuters/L. Kuegeler)

Dortmund washerehekea bao la Jadon Sancho

Paco Alcacer alifunga mabao mawili na wengine walioandikisha majina yao katika daftari la wafungaji ni Jadon Sancho, Marco Reus na Julian Brandt ambaye alifunga katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa BVB baada ya kujiunga nao katika dirisha la uhamisho lililopita kutoka Bayer Leverkusen.

Augsburg walifungiwa bao la kufutia jasho na Florian Niederlechner.