Bayern mabingwa mara saba mfululizo | Michezo | DW | 20.05.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bayern mabingwa mara saba mfululizo

Bayern Munich wamelinyakua taji lao la ishirini na tisa la Bundesliga katika siku ya mwisho ya mechi za Ligi Kuu ya Ujerumani baada ya kuiaibisha Eintracht Frankfurt magoli sita kwa moja.

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa nyumbani wa Bayern Allianz Arena.

Mustakabali wa kocha Niko Kovac kwa sasa bado haujulikani hapo Bayern licha ya kulibeba taji hilo la Bundesliga na kuweka rekodi ya kuwa mtu wa pili kuebuka bingwa wa taji hilo kama mchezaji na kama kocha baada ya Franz Beckenbauer.

Borussia Dortmund wamemaliza msimu kwenye nafasi ya pili baada ya kupata ushindi wa 2-0 uwanjani Borussia Park walipokuwa wakichuana na wenyeji Borussia Moenchengladbach.

Dortmund walifungiwa mabao yao na Jadon Sancho na nahodha Marco Reus.