Barcelona yatwaa ubingwa ikimuaga Iniesta | Michezo | DW | 21.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Barcelona yatwaa ubingwa ikimuaga Iniesta

Ilikuwa wikiendi ambayo Barcelona ilitwaa ubingwa wa La Liga huku pia ligi hiyo ya kandanda Uhispania ikiwaaga wachezaji nguli Andres Iniesta na Fernando Torres

Barca walishindwa mchuano mmoja pekee msimu mzima wakati wakibeba ubingwa wa Uhispania ambapo walikuwa na pengo la pointi 14 kileleni mbele ya nambari mbili Atletico Madrid na 17 mbele ya nambari tatu Real Madrid. Lavencia walichukua nafasi ya nne na tikiti ya mwisho ya Champions League. Lionel Messi alimaliza msimu akiwa mfungaji bora na mabao 34. Villareal, Real Betis na Sevilla watacheza Europa league. Deportivo la Coruna, Las Palmas na Malaga zilishushwa daraja

Na wakati msimu wa La liga ukikamilika, Fernando Torres aliiambia kwaheri klabu yake ya tangu utotoni Atletico Madrid, kisha saa chache baadaye, Andres Iniesta akafunga pazia la misimu 16 aliyoichezea Barcelona. Iniesta alibubujikwa machozi wakati akitoa hotuba ya kuaga uwanjani Camp Nou

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Mohamed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com