1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona yamtimua kocha wake kufuatia kichapo cha Bayern

18 Agosti 2020

Klabu ya Barcelona imemtimua kocha wake Quique Setien, siku chache baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha magoli 8-2 kutoka kwa Bayern Munich katika michuano ya klabu bingwa balani Ulaya Champions League

https://p.dw.com/p/3h6qu
Fussball l Neuer Trainer bei FC Barcelona - Quique Setien
Picha: Reuters/A. Gea

Vyombo vya habari mjini Barcelona vimeripoti kuwa rais wa klabu hiyo Josep Bartomeu yumo kwenye mazungumzo na Ronald Koeman anayetajwa kuchukua mikoba. Koeman amekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi tangu mwaka 2018. Setien alichaguliwa kuifandisha Barcelona mwezi Januari lakini ameshindwa kuchukua taji la La liga na kisha kupokea kipigo cha magoli 8 kutoka Bayern . Wakati huo huo Inter Milan iimetinga fainali ya Europa League baada ya kuichapa Shakhtar Donetsk mabao 5-0 katika mchezo wa nusu fainali. Klabu hiyo ya Italia sasa itavaana na Sevilla katika mchezo wa fainali utakaofanyika Ijumaa mjini Cologne Ujerumani.