Barcelona yaipiku Real Madrid katika El Clasico | Michezo | DW | 23.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Barcelona yaipiku Real Madrid katika El Clasico

Vilabu viwili vikuu nchini Uhispania viliteremka uwanjani jana usiku katika mchuano mkali wa watani wa jadi maarufu kama El Clasico.

Matokeo rasmi yalikuwa ni Barcelona 2, Real Madrid 1. Lakini kwa wengine, huenda matokeo yalikuwa ni Cristiano Ronaldo 1, Messi 0. El Classico huwa ni tamasha ambalo wengi hutaka kuona ubabe wa washambuliaji CR7 wa Real MADRID na Lionel Messi wa Barcelona na hapo jana CR7 alifunga goli wakati Messi akiambulia patupu.

Hata hivyo goli safi la Luis Suarez liliimarisha uongozi wa Barca kileleni mwa La liga na pengo la pointi nne dhidi ya nambari mbili Real Madrid. Jeremy Mathieu alifungua ukurasa kabla ya CR 7 kujibu kwa kufunga bao lake la 47 la msimu. Kisha Suarez akatikisa wavu na kufunga kazi. Ni mpambano ambaoulitazamwa na zaidi ya watu milioni 400 kote ulimwenguni – na wengine 98,000 ndani ya uwanja wa Camp Nou.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com