Barcelona mabingwa La Liga | Michezo | DW | 29.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Barcelona mabingwa La Liga

Barcelona tayari wameshalinyakua taji lao la 26 la Ligi Kuu ya Uhispania La Liga kwa kuwalaza Levante bao moja bila jawabu siku ya Jumamosi.

Lionel Messi ndiye aliyekuwa mfungaji wa goli hilo la pekee lililowahakikishia ubingwa.

Kocha wa Barca Ernesto Valverde alikuwa na haya ya kusema baada ya mechi hiyo.

"Nina wachezaji wazuri sana, hiki ni kikundi cha wachezaji ambao wanaweza kuwa na siku nzuri au mbaya ila wanaweza kufanya mambo yakawa rahisi sana kwako," alisema Valverde.

Real Madrid ambao wanaishikilia nafasi ya tatu kwenye jedwali la La Liga walipoteza mechi yao dhidi ya Rayo Vallecano walipofungwa moja bila Jumapili. Kocha Zinedine Zidane aliwashambulia wachezaji wake baada ya kipigo hicho.

Fußball Champions League l Real Madrid gegen Ajax Amsterdam (Reuters/S. Vera)

Mlinda lango wa Madrid Thibaut Courtois

"Kwa kawaida mimi huwatetea wachezaji wangu lakini leo siwezi, ndio ukweli huo. Hatuwezi kucheza hivi, lakini si wao tu, hata mimi mwenyewe ni wa kulaumiwa kwasababu mimi ndiye ninayeiunda timu, mimi ndiye ninayezungumza nao lakini mwishowe tulifanya tofauti kabisa ya kile tulichozungumza. Kwa hiyo ni kitu ambacho itanibidi nikiangazie upya tena," alisema Zidane.