1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona hoi tena

7 Desemba 2020

Kocha wa miamba wa Uhispania Barcelona Ronald Koeman amewashambulia wachezaji wake kwa kukubali goli kwa urahisi walipofungwa 2-1 na Cadiz Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania La Liga.

https://p.dw.com/p/3mKIo
Fußballspieler Lionel Messi nach niederlage gegen Bayern München 2020
Picha: picture-alliance/AP Images/M. Fernandez

Alvaro Negredo ndiye aliewafungia Cadiz hilo goli la ushindi baada ya makosa kadhaa yaliyofanywa na wachezaji wa Barcelona. Na sasa Koeman anasema yote hayo yametokea kwasababu wachezaji wake hawakuwa makini.

Spanien F.C. Barcelona | Neuer Coach Ronald Koeman
Kocha wa Barcelona Ronald KoemanPicha: picture-alliance/AA/A. Puig

"Kwa kweli nafikiri ni hatua iliyoturejesha nyuma sana katika harakati zetu za kutaka kujaribu tulishinde taji. Lazima tuitazame tena mechi hii ambayo matokeo ya mwisho yanavunja moyo sana na ni lazima tukubali na tujaribu kuwa bora zaidi. Tuko pointi 12 nyuma ya Atletico Madrid ambayo kwa sasa ni timu nzuri sana, na pointi hizo ni nyingi ila lazima tuendelee kufanya bidii. Bado tuna mechi kadhaa za kucheza ila ni kweli kwamba tusipojitahidi na kuuboresha mtazamo wetu wa mechi, basi kama timu hatutaimarika. Tunastahili kupata matokeo nyumbani na ugenini," alisema Koeman.

Kwa sasa Barcelona wanaishikilia nafasi ya tisa katika msimamo wa La Liga huku Atletico Madrid wakiongoza na alama ishirini na sita halafu Real Sociedad wako alama moja nyuma yao katika nafasi ya pili na Villareal ni watatu wakiwa na pointi ishirini na moja na mabingwa watetezi Real Madrid ni wanne na pointi ishirini.