Barca walazwa, Madrid wapaa | Michezo | DW | 27.01.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Barca walazwa, Madrid wapaa

Kwenye La Liga huko Uhispania mabingwa Barcelona walipoteza mechi yao ya kwanza chini ya kocha wao mpya Quique Setien walipokuwa wakichuana na Valencia.

Barca walishindiliwa mabao mawili kwa bila katika mechi ambayo hao wenyeji wao Valencia ndio walioshambulia mno.

Baada ya kipigo hicho kocha Setien amekiri kwamba anastahili kulaumiwa kwa mchezo mbaya wa hiyo timu yake mpya.

"Ni kweli kwamba kuna baadhi ya vitu ninavyowafunza ambavyo wachezaji hawajavielewa vizuri au labda sisi kama makocha hatujavieleza vizuri. Ukweli ni kwamba hayo tumeyaona leo na sidhani kama yeyote kai yetu anafurahia, si wachezaji wala sisi makocha," alisema Setien.

Fußball UEFA Champions League FC Brügge vs Real Madrid (AFP/J. Thys)

Mchezaji wa Real Madrid Vinicus Junior

Matokeo hayo yanamaanisha kwamba Barcelona wameondolewa kutoka kwenye nafasi ya kwanza na mahasimu wao Real Madrid ambao walipata ushindi mwembamba wa moja bila jana walipokuwa wakicheza na Real Valladolid.

Madrid sasa wako kileleni na arubaini na sita pointi tatu mbele ya Barcelona kisha Sevilla ni wa tatu na pointi thelathini na nane wakifuatwa na Getafe wenye alama thelathini na sita.

Valencia licha ya kuwaangusha miamba hao wa La Liga wao wanaishikilia nafasi ya saba wakiwa na pointi thelathini na nne.