1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la wawakilishi lakamilisha hoja za kumshtaki Trump

Iddi Ssessanga
12 Februari 2021

Waendesha mashtaka wa baraza la wawakilishi wamefunga hoja zao katika kesi ya mashtaka dhidi ya Donald Trump, kwa kuliomba baraza la seneti kumtia hatiani kwa kuchochea shambulio baya la Januari 6 dhidi ya bunge.

https://p.dw.com/p/3pFVX
USA | Impeachment-Prozess gegen Trump | Diana DeGette
Picha: AP Photo/picture alliance

Wasimamizi wa mashtaka hayo kutoka Baraza la Wawakilishi wamefunga kesi yao baada ya siku mbili za hoja zilizohusisha maneno ya Trumpmwenyewe, na masaa kadhaa ya kuonyesha picha za video kutoka shambulio dhidi ya makao ya bunge na wafuasi wa Trump, ambao walikuwa wanataka kuzuwia zoezi la uhakiki wa ushindi wa mdemocrat Joe Biden katika uchaguzi wa Novemba 3.

Mawakili wa Trump wataanza utetezi wao leo Ijumaa, wakihoji kwamba rais huyo wa zamani hawezi kuwajibishwa binafsi kwa uvamizi wa bunge. Wamehoji pia kabla kwamba mashtaka hayo hayana msingi kikatiba kwa sababu Trump hivi sasa hayuko tena madarakani, inagwa hoja hiyo ilitupiliwa mbali na Seneti mapema wiki hii.

USA | Impeachment-Prozess gegen Trump | Jamie Raskin Rede
Kiongozi wa timu ya mashtaka Jamie Raskin.Picha: U.S. Senate TV via REUTERS

"Tunawaomba kwa heshima na taadhima mumtie hatiani rais Trump kwa makosa ambayo ana hatia kubwa kwayo," alisema mwakilishi wa chama cha Democratic Joe Neguse, mmoja wa wasimamizi tisa wa mashtaka kutoka baraza la wawakilishi.

Soma pia: Baraza la Seneti lapiga kura kuendelea na kesi ya Trump

"Kwa sababu msipofanya hivyo, iwapo tutajifanya kama vile hili halikutokea -- au mabaya zaidi, tukiliacha kupita bila kutolewa majibu-- nani anatasema halitotokea tena?"

Jamie Raskin, kiongozi wa timu ya timu ya mashtaka, aliwakumbusha maseneta 100 wanaokaa kama wazee wa baraza juu ya kiapo chao cha kutoa haki bila upendeleo.

Matumaini finyu ya Trump kutiwa hatiani

Mapema, rais Biden alisema ushahidi wa vidio dhidi ya mtangulizi wkae mwenye umri wa miaka 74 uliwasilishwa mbele ya Seneti unaweza kubadili baadhi ya wabunge. Lakini licha ya kile ambacho baadhi ya Warepublican wamekitaja kuwa kesi nzito ya mashtaka, Trump anabaki kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama, hali inayofanya kuwa vigumu sana kumtia hatiani.

USA | Trump Impeachment | Video Evakuierung Vizepräsident Mike Pence
Picha kutoka mkanda wa vidio ikumuonyesha makamu wa rais Mike Pence akiondolewa baada ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge, Januari 6.Picha: Senate Television/AP/picture alliance

Ili hilo kufanyikaa itahitajika wingi wa theluthi mbili ya wanachama 100 wa baraza la seneti, hii ikimaanisha kuwa Warepublican 17 watahitajika kuungana na Wademocrat 50 wa baraza hilo. Machafuko hayo ya Januari 6 yaliripuka baada ya Trump kufanya mkutano mkubwa karibu na ikulu ya White House, akisisitiza isivyokweli kwamba aliporwa ushindi wake.

Soma pia: Trump akataa wito wa kutoa ushahidi bungeni

Baada ya kuagizwa na Trump kuandamana kuelekea bunge, ambako wabunge wakati huo walikuwa wanaidhinisha ushindi wa Biden, kundi la wafuasi hao wa Trump walivinja vizuwizi vya polisi, na kuanza kufanya uhairibifu mkubwa, katika machafuko yaliosababishwa vifo vya watu watano.

Chanzo:Mashirika