1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Baraza la Usalama lataka Iran iache kuzilenga nchi za Ghuba

12 Machi 2026

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa Iran kusitisha mashambulizi dhidi ya nchi za Ghuba, kupitia azimio ambalo halikutaja mashambulizi ya Marekani au Israel dhidi ya Iran.

https://p.dw.com/p/5AD8g
USA New York 2026 | Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakutana baada ya mashambulizi kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakutana baada ya mashambulizi kati ya Marekani na Israel dhidi ya IranPicha: Cristina Matuozzi/Sipa USA/picture alliance

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa Iran kusitisha mashambulizi dhidi ya nchi za Ghuba, kupitia azimio ambalo halikutaja mashambulizi ya Marekani au Israel dhidi ya Iran.

Azimio hilo, lililopitishwa kwa kura 13 huku nchi mbili zikijizuia, linataka kusitishwa mara moja kwa mashambulizi yote yanayofanywa na Iran dhidi ya Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan.

Pia linalaani hatua au vitisho vyovyote vinavyofanywa na Tehran, vinavyolenga kufunga au kuzuia safari za meli za kimataifa kupitia Mlango Bahari wa Hormuz.

Balozi wa Iran, Amir Saeid Iravani, alisema kupitishwa kwa azimio hilo ni matumizi mabaya ya wazi ya mamlaka ya Baraza la Usalama kwa ajili ya kulinda maslahi ya kisiasa ya Marekani na Israel.