1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la katiba Chad lakataa kufuta matokeo ya uchaguzi

16 Mei 2024

Baraza la Katiba nchini Chad limeyatupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na wagombea wawili walioshindwa kwenye uchaguzi wa rais, ya kutaka matokeo ya uchaguzi huo yabatilishwe.

https://p.dw.com/p/4fwqD
Mahamat Deby Itno wa  Chad
Mahamat Deby Itno / ChadPicha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Baraza la  Katiba nchini Chad  limeyatupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na wagombea wawili walioshindwa kwenye uchaguzi wa rais, ya kutaka matokeo ya uchaguzi huo yabatilishwe.

Baraza hilo limesema wagombea hao wameshindwa kutowa ushahidi kuunga mkono madai yao kwamba ulifanyika udanganyifu.

Tume ya uchaguzi wiki iliyopita ilimtangaza mshindi rais wa mpito Mahamat Idriss Deby wa uchaguzi huo wa rais, kwa kupata asilimia 61.3 huku Masra akichukua nafasi ya pili kwa kujipatia asilimia 18.53 ya kura, kulingana na matokeo ya awali.