BAIDOA:Mapigano yazuka Idale Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAIDOA:Mapigano yazuka Idale Somalia

Vikosi vinavyotii mahakama za kiislamu huko Somalia vimepambana mapema leo asubuhi na wanajeshi wa serikali ya mpito inayoungwa mkono na wanajeshi wa Ethiopia katika eneo la Idale.

Mapambano hayo yamefanyika siku ikiwa ni siku moja baada ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa na mahakama hizo wa kuwataka wanajeshi wa Ethiopia waondoke katika ardhi ya Somalia.

Habari hizo zimethibitishwa na maafisa katika wizara ya ulinzi ingawa hawakuweza kusema idadi ya watu waliojeruhiwa au kuuwawa kwenye mapigano hayo.

Mahakama za kiisalamu ambazo zinadhibiti maeneo mengi ya kusini na kati mwa Somalia hivi karibuni walitangaza vita takatifu dhidi ya wanajeshi wa Ethiopia.Wadadisi wameonya kwamba vita nchini Somalia vinaweza kusambaaa katika eneo zima la pembe ya Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com