1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Atletico Madrid wazidi kutamba La Liga

25 Januari 2021

Mwishoni mwa wiki kulipigwa mechi za Ligi Kuu La Liga, Uhispania na Atletico Madrid wakahakikisha kwamba wanaendelea kuiongoza ligi hiyo baada ya kutoa ushindi wa 3-1 walipokuwa wakichuana na Valencia

https://p.dw.com/p/3oNuf
Atletico Madrid v Bayern Munich | Torjubel zum 1:0 durch Joao Felix (Atletico Madrid, 7)
Picha: Benjamin Soelzer/Eibner/imago images

Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Luis Suarez alionyesha makali yake kwa kuwa miongoni mwa waliocheka na wavu.

Real Madrid walipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Alaves nao Barcelona waliomkosa Lionel Messi ambaye ana marufuku, wakapata ushindi wa 2-0 walipokuwa wakicheza na Eibar.

Kwa sasa Atletico wako uongozini na pointi 47 Real Madrid nao pointi walizo nazo ni 40 kisha Barcelona ni wa tatu na pointi 37 huku Sevilla wakikamilisha nne bora na pointi 36.