1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Athari za ukame Tana River, Kenya

Faiz Abdallah Musa14 Septemba 2021

Ukame unaoendelea kulikumba jimbo la Tanariva katika Pwani ya Kenya umeathiri vibaya shughuli za masomo ambapo kwa sasa mamia ya wanafunzi hawaudhurii shule kwa sababu ya kuhama kwenda kutafuta maji. Faiz Musa na taarifa kamili.

https://p.dw.com/p/40IL5

Hali katika eneo hili imezidi kuwa mbaya licha ya jitihada mbali mbali za kusaidia jamii hizo kwa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na mifugo. Kulingana na mbunge wa Garsen, Ali Wario, shule za msingi za Assa, Odoganda, na Kone-Bisadi idadi ya wanafunzi wamepungua huku shule ya Assa ikifunga bweni kutokana na ukali wa ukame huo na kupotea kwa maji.

Makali ya ukame huo umezilazimisha jamii nyingi kuhama vijiji vyao ili kutafuta maji na malisho kwa mifugo yao katika eneo la chemichemi la bonde la Mto Tana, Tana Delta, zaidi ya kilomita kumi kutoka kwa mkaazi yao huku walimu nao pia wakilazimika kusitisha masomo mara kwa mara ili nao watafute maji.

Kutokana na wafugaji kuelekea katika eneo la Tana Delta kuliko na chemichemi za maji, idara ya usalama inahofia kuzuka kwa mafarakano baina ya wafugaji hao na wenyeji ambao ni wakulima. Naibu kamishna wa Tana Delta, William Nasongo, amezitaka jamii hizo kusaidiana wakati huu na iwapo mizozo itaanza kuchipuka basi wawahusishe maafisa wa idara ya usalama.

Kulingana na mamlaka ya kudhibiti ukame nchini Kenya, NDMA, Zaidi ya familia elfu sitini na tatu zinakumbwa na baa la njaa na uhaba wa maji katika jimbo hilo, Abdi Musa ni mkurugenzi wa mamlaka hiyo.