1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Historia

Asili ya Afrika: Mfahamu Ahmed Baba

Daniel Gakuba
4 Aprili 2018

Mji wa Timbuktu wa Kaskazini mwa Mali uliwahi kusifiki kwa ustawi wake. Karne ya 14 mji huo ulio pembezoni mwa Jangwa la Sahara ulikuwa kituo muhimu cha wanazuoni wa Kiislamu na kituo cha shughuli za biashara. Wafanyabiashara walikutana hapo kununua chumvi, dhahabu, pembe za ndovu na watumwa. Miongoni mwa watu waliochangia katika umaarufu wa Timbuktu ni msomi mkubwa wa Kiafrika, Ahmed Baba.

https://p.dw.com/p/2vUbN