1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASCHGABAT: Waziri Steinmeier amewasili Turkmenistan

2 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwg

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amewasili Turkmenistan.Hicho ni kituo cha tatu katika ziara yake ya hivi sasa katika nchi za Asia ya Kati.Steinmeier amepanga kukutana na waziri mwenzake Rashid Meredov na pia rais Saparmurat Nijasov alieitenga nchi yake na jumuiya ya kimataifa.Serikali ya Turkmenistan inalaumiwa vikali kuwa inakiuka haki za binadamu na kukandamiza kila aina ya upinzani.Azma ya ziara ya waziri Steinmeier ni kutazama njia za kuboresha ushirikiano kati ya nchi za Asia ya Kati na Umoja wa Ulaya.Ujerumani mwezi wa Januari itashika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka.Ziara ya Steinmeier imeshampeleka Kazakhstan na Uzbekistan.Vituo vya mwisho katika ziara yake ya nchi za Asia ya Kati ni Tajikistan na Kyrgyzstan.